Shajara ya Uokoaji nchini Uturuki: Hakuna muda wa kusitasita, twende kwenye eneo la tetemeko la ardhi la Malatya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 10, 2023

Baada ya kusafiri kwa zaidi ya saa 30, na kupita Guangzhou, Dubai, na Istanbul, kikosi cha kwanza cha uokoaji cha Anga Buluu cha Mkoa wa Jiangsu wa China kinachokwenda Uturuki, kiliwasili Uwanja wa Ndege wa Adana wa nchi hiyo tarehe 9, Februari saa 6:45 usiku, na mimi ni mmoja wa waokoaji wa kikosi hicho.

Kabla ya kufunga safari, nilihisi watu wa familia yangu wana wasiwasi na kutopenda mimi kuondoka, lakini tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki limegusa mioyo ya watu wote, na kuhitaji msaada wa vikosi vya uokoaji duniani.

Ingawa tuliandaa mipango mingi tukiwa njiani, lakini baada ya kuwasili Uturuki, mambo mengi yaliyotokea kwa dharura yalizidi mipango yetu. Baada ya kushuka kutoka kwenye ndege, mara moja tuliambiwa kuwa, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa zaidi ya 5 kwa kipimo cha Ritcher lilikuwa limetokea hivi punde, na hali ya hewa ilileta changamoto kwa kazi za uokoaji.

Tarehe 9, Februari saa 9:00 alfajiri kwa saa za Ankara, kikosi chetu cha kwanza kilipokea– kazi ya kwenda kwenye eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi la Malatya. Eneo hilo ni moja ya miji iliyoathirika vibaya zaidi katika tetemeko la ardhi Kusini Mashariki mwa Uturuki, ambapo kuna upungufu mkubwa wa mahitaji, na kazi za uokoaji zinakabiliwa na changamoto kubwa. Hadi hivi sasa bado hakuna kikosi cha kimataifa kinachofanya uokoaji huko. Tumejulishwa kuwa, Wachina wanaoishi nchini Uturuki, wakalimani na wengine wa kujitolea pia wamejiandaa ili kusaidia kikosi cha uokoaji cha Anga Buluu kutoka China. Hakuna muda wa kusitasita, fanya haraka, kwenda kwenye eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi la Malatya! 

Mkuu wa Kikosi cha Uokoaji cha Anga Buluu cha mji wa Yangzhou, Mkoa wa Jiangsu wa China Zhang Yunlu na mwenzake Dai Xiaodong wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Istanbul. Picha inatolewa na Zhang Yunlu.

Gari la Huduma za Uokoaji la China nchini Uturuki. Picha imetolewa na Zhang Yunlu.

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha