Hifadhi ya Mto Manjano kujaza maji kwenye mto mkubwa wa Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2023

Picha iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha watu wakitembea kwa kufuata kando ya Mto Yongding wakati wa machweo ya jua katika Eneo la Daxing, Beijing, China, Mei 30, 2021. (Xinhua/Li Xin)

TAIYUAN - Kampuni ya Wanjiazhai Water Holding ya China imesema siku ya Jumanne kuwa, Bwawa kubwa la Wanjiazhai lililoko katikati mwa Mto Manjano, litaendelea kujaza maji mwaka huu kwenye Mto Yongding, mto mkubwa muhimu unaopita katika Mji wa Beijing.

Maji yenye jumla ya mita za ujazo milioni 165 yataelekezwa kutoka Bwawa la Wanjiazhai hadi Mto Yongding mara mbili, katika majira ya mchipuko na mpukutiko , ili kusaidia kurejesha mazingira ya kiikolojia katika eneo la Beijing-Tianjin-Hebei.

Ndani yake, maji yenye mita za ujazo karibu milioni 100 yataelekezwa wakati wa majira ya mchipuko kwa kasi ya wastani ya mita za ujazo 10 kwa sekunde.

Eneo la mtiririko wa maji ya Mto Yongding ni moja ya maeneo muhimu ya hifadhi ya maji na kizuizi na ukanda wa kiikolojia wa Beijing na maeneo ya jirani. Kiasi cha maji yaliyojazwa tena kimezidi mita za ujazo bilioni 1.1 kutoka Mwaka 2017 hadi 2022.

Mto Yongding unaotiririka kupita Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China, Mkoa wa Shanxi, Mkoa wa Hebei, na miji ya Beijing na Tianjin, ukiwa na urefu wa kilomita 759. Sehemu ya mto huo ya Beijing ina urefu wa kilomita 170, na eneo la mtiririko wa maji ni lenye kilomita za mraba 3,200.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha