Tanzania yapanga kuzalisha umeme wa megawati 5,000 kufikia 2025

(CRI Online) Februari 16, 2023

Waziri wa Nishati wa Tanzania Bw. January Makamba amesema hadi kufikia Mwaka 2025 Tanzania itakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wenye nguvu za megawati 5,000 kwa mujibu wa miradi inayotekelezwa sasa.

Akiongea Ikulu mjini Dar es salaam kwenye hafla ya utiaji saini wa mikataba ya uimarishaji wa gridi ya taifa, Bw. Makamba amesema kwa sasa Tanzania inazalisha umeme wa megawati 1,700 ambao hautoshi kwa mahitaji ya nchini humo, lakini hadi kufikia Mwaka 2025 uzalishaji wa umeme nchini Tanzania utakuwa mara tatu zaidi ya uzalishaji wa umeme uliopo sasa.

Pia amesema kwa sasa Tanzania ina njia kuu za kusafirisha umeme zenye urefu wa kilometa 6,000 lakini mahitaji ni kilometa 12,000.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha