Mkuu wa UNHCR na Rais Samia Suluhu wa Tanzania wajadili suala la kuwarejesha makwao wakimbizi

(CRI Online) Februari 16, 2023

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limepongeza utamaduni wa muda mrefu wa Tanzania wa kukaribisha wakimbizi na kuhimiza kuendelea kwa juhudi za kushughulikia mahitaji ya wale wanaokimbia migogoro.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Bw. Filippo Grandi, ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akikutana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, na amesisitiza dhamira ya UNHCR ya kusaidia wakimbizi kurejea salama kutoka nchi walizopata hifadhi, na baadaye kuunganishwa tena na jamii.

Kwenye mkutano wao wamejadili hatua iliyofikiwa katika kuweka mazingira mazuri nchini Burundi kwa ajili ya wakimbizi kurejea nyumbani.

Takriban wakimbizi 248,000 na wanaotafuta hifadhi, hasa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaishi nchini Tanzania.

Bw. Grandi amesema UNHCR inakaribisha tangazo la hivi karibuni la Umoja wa Ulaya (EU) la kutoa Euro milioni 40 katika miaka ijayo kwa washirika wake kusaidia Suluhu nchini Burundi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha