Moscow yawafukuza wafanyakazi wanne wa ubalozi wa Austria katika hatua ya kulipiza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2023

Watu wakitembea karibu na jengo la Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia huko Moscow Machi 28, 2022. (Xinhua/Bai Xueqi)

MOSCOW - Moscow imetangaza wafanyakazi wanne wa Ubalozi wa Austria nchini Russia kuwa "wasiokaribishwa kuingia" katika hatua ya kulipiza kisasi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema Alhamisi.

Wizara hiyo ilimwita Balozi wa Austria nchini Russia, Werner Almhofer siku ya Alhamisi kupinga uamuzi wa Serikali ya Austria kuwafukuza wafanyakazi wanne kutoka kwenye ubalozi wa Russia, imesema na kuongeza kuwa wanadiplomasia wa Austria lazima waondoke Russia ifikapo Februari 23.

“Hatua ya Austria isiyo ya kirafiki na isiyo na sababu inasababisha uharibifu mkubwa kwa uhusiano wa nchi mbili,” imesema wizara hiyo.

Austria ilitangaza wanadiplomasia wawili wa Ubalozi wa Russia na wanadiplomasia wawili wa Ujumbe wa Kudumu wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa "wasiokaribishwa kuingia" mnamo Februari 2.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha