

Lugha Nyingine
Mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika Kusini yaendelea kuharakishwa
Mkutano wa tatu wa ngazi ya juu kuhusu utaratibu wa mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika Kusini, umefanyika mjini Cape Town, ambapo pande mbili zimefanya majadiliano ya kina kuimarisha mawasiliano hayo na kusaini makubaliano matatu yanayohusu sekta za elimu, sayansi na teknolojia, na afya.
Mkutano huo umefanyika wakati China na Afrika Kusini zimeadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi, na wakati Afrika Kusini inashika uenyekiti wa kundi la BRICS kwa mwaka huu. Wachambuzi wanaamini kuwa mkutano huo utaongeza nguvu ya msukumo kwenye mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Katika miaka ya hivi karibuni pande mbili zimekuwa na shughuli mbalimbali za mawasiliano kati ya watu na mawasiliano ya kitamaduni na kupata mafanikio makubwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma