

Lugha Nyingine
China yasaidia Watoto wa Kenya kutimiza ndoto ya Masomo
Wanafunzi katika Shule ya MCEDO Beijing huko Nairobi, Kenya, wakipozi ili kupiga picha ya pamoja tarehe 14, Februari. Wafanyabiashara wa China wamesaidia wanafunzi kwenye shule hiyo kwa kukarabati madarasa na kutoa msaada wa chakula. Dong Jianghui/Xinhua
Hagai Otieno, ambaye alizaliwa na kulelewa Mathare, eneo la pili la makazi yasiyopangwa vizuri kwa ukubwa wake mjini Nairobi, alikuwa na wasiwasi kwamba huenda atalazimika kuacha masomo kama ndugu zake wakubwa.
Baba yake, ambaye ni kibarua na mtu pekee anayehudumia familia, hushindwa kununua chakula kwa familia, achilia mbali kuweza kumudu malipo ya karo ya watoto wake.
Sasa, Otieno anathubutu kuota ndoto kubwa zaidi. Amemaliza masomo ya sekondari ya upili mwaka jana na ataingia kwenye chuo kikuu nchini China baadaye mwaka huu kusoma uhandisi wa umeme, shukrani kwa ufadhili wa masomo uliotolewa na serikali ya China.
Anashukuru sawasawa jumuiya ya Wachina na Shirika la Uchumi na Biashara la China-Kenya kwa uungaji mkono wao bila ya kulegalega kwa Shirika la Elimu na Maendeleo ya Jumuiya ya Mathare Shule ya Beijing (MCEDO), ambako alisoma huko.
Tangu shule hiyo ilipoanzishwa Mwaka 2007, kutokana na msaada wa Ubalozi wa China nchini Kenya, shirikisho hilo limetoa chakula, vifaa vya masomo na samani kila baada ya kipindi maalumu, na kukarabati madarasa kila inapohitajika.
Hivi sasa Shule ya MCEDO Beijing ina shule ya kimsingi yenye wanafunzi 370, na sekondari yenye wanafunzi 156. Zaidi ya wanafunzi 1,500, ambao wote wanatoka makazi yasiyopangwa vizuri, wamemaliza masomo yao ya sekondari. Baadhi yao wanasomea shahada ya kwanza ya chuo kikuu au wameanza kufanya kazi ili kuunga mkono familia zao, anasema Benedict Kiage, mwalimu mkuu wa shule hiyo.
Wanafunzi kadhaa wamekiambia chombo cha habari cha China Daily kuwa, hupewa vyakula vingi sana shuleni kiasi kwamba huchukua chakula kwa wazazi na ndugu zao nyumbani.
Zhang Yijun, konsula wa ubalozi wa China amesema, mradi huo wa chakula na madarasa yaliyokarabatiwa vitatoa motisha kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma