Ukweli wa Mambo: Mtego wa madeni? Mambo ya kujua kuhusu Ushirikiano kati ya China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2023

Kwa mara nyingine tena, maofisa wa Serikali ya Marekani wanarudia hoja ya "mtego wa madeni" kwenye ziara wanazofanya barani Afrika, wakidai kuwa China inazibebesha nchi za Afrika madeni yasiyo endelevu. Je, hoja yao ni sahihi au hicho kinachoitwa mtego wa madeni wa China ni uongo uliotungwa na Marekani na nchi za Magharibi ili kukwepa wajibu na lawama zao? Huu hapa ni ukweli wa mambo ambao People's Daily imekusanya.

Wakopeshaji wa kibiashara na wa kimataifa ndio wakopeshaji wakubwa wa deni la nje la Afrika, wakichukua karibu robo tatu ya madeni ya jumla ya nje ya Afrika

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Benki ya Dunia, kati ya deni lote la nje la dola bilioni 696 la serikali 49 za Afrika zenye takwimu, takriban robo tatu inadaiwa na taasisi za kimataifa na wakopeshaji wa kibinafsi wasio Wachina. Shirika la Debt Justice limebaini kuwa kwa nchi 24 za Afrika zenye mzigo mkubwa wa deni, wastani wa sehemu ya malipo yao ya deni la nje kutoka Mwaka 2022 hadi 2028 kwa wadai wa kibinafsi wasio Wachina na wadai wa kimataifa inakadiriwa kuwa 32% na 35% .

Kwa mfano, taasisi za fedha za kimataifa zinachangia asilimia 24 ya deni la nje la Zambia, wakati wakopeshaji wa kibiashara wa nchi za Magharibi wanachukua asilimia 46. Kwa pamoja, wanashikilia sehemu kubwa ya deni la nje la Zambia.

Kwahiyo, Marekani na nchi za Magharibi zinapaswa kuwajibika kwa matokeo ya kuzifanya baadhi ya nchi kuingia kwenye "mtego wa madeni."

Ushirikiano kati ya China na Afrika umeleta manufaa yanayoonekana kwa nchi za Afrika na watu wake

Tatizo la deni la Afrika ni suala la maendeleo. Ushirikiano wa kifedha wa China na Afrika ni hasa katika maendeleo ya miundombinu na uwezo wa uzalishaji, na unalenga kuimarisha uwezo wa Afrika wa kujiendeleza kwa kujitegemea na kwa uendelevu.

Tokea mwanzoni mwa karne hii, China imejenga zaidi ya kilomita 6,000 za reli, kilomita 6,000 za barabara, karibu bandari 20, na zaidi ya vituo 80 vya umeme barani Afrika, na kusaidia kujenga zaidi ya hospitali na zahanati 130, zaidi ya shule 170, viwanja vya michezo 45 na zaidi ya miradi 500 ya kilimo huko. Miradi hii imechangia zaidi katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika na kuboresha maisha ya watu, na imethaminiwa sana na nchi na watu wa Afrika.

Kwa mfano, Reli ya Kenya ya Mombasa-Nairobi ya Standard Gauge (SGR) imekuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kenya na kuboresha maisha ya watu tangu ilipoanza kufanya kazi miaka mitano iliyopita, na kuchangia zaidi ya asilimia 2 katika Pato la Taifa la Kenya na kutengeneza karibu nafasi za kazi 50,000 nchini Kenya. Zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wa reli hiyo ni wenyeji.

Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, ikiwa miradi yote ya miundombinu ya usafiri ya ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) itatekelezwa ifikapo Mwaka 2030, BRI itazalisha dola za kimarekani trilioni 1.6 katika mapato kila mwaka, au 1.3% ya Pato la Jumla Taifa la kimataifa.

China ndiyo mchangiaji mkubwa zaidi kwenye Mpango wa Kusimamisha Madeni wa G20

China siku zote imekuwa ikijitolea kuisaidia Afrika kupunguza mzigo wake wa madeni, inashiriki kikamilifu katika Mpango wa Kusitisha kwa muda malipo ya Madeni wa Kundi la 20 (G20), kusaini makubaliano au kufikia makubaliano na nchi 19 za Afrika kuhusu msamaha wa deni na ni nchi inayoongoza kwa kusitisha kwa muda malipo mengi zaidi ya deni miongoni mwa wanachama wa G20. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha