

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa UN asema Marekani na Russia zinapaswa kurudisha utekelezaji wa mkataba wao wa upunguzaji silaha za nuklia
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumanne ametoa wito kwa Marekani na Russia kurudisha utekelezaji kamili wa Mkataba Mpya wa Kimkakati wa Kupunguza Silaha (New START)).
Alipoulizwa kuhusu maoni ya Guterres kwa tangazo la Rais wa Russia Vladimir Putin kwamba nchi yake itasitisha ushiriki wake katika mkataba huo wa New START unaolenga kupunguza silaha za nyuklia, Msemaji wa Guterres Stephane Dujarric amesema Jumatano kuwa msimamo wa katibu mkuu ni kwamba Marekani na Russia zinapaswa kurudisha utekelezaji kamili wa mkataba bila kuchelewa.
"New START na mikataba iliyofuatana ya pande mbili juu ya upunguzaji wa kimkakati wa silaha za nyuklia kati ya nchi hizo mbili imetoa usalama siyo tu kwa Russia na Marekani, bali pia kwa jumuiya nzima ya kimataifa," amesema Dujarric.
Dujarric ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba, Dunia isiyo na udhibiti wa silaha za nyuklia ni Dunia hatari zaidi na isiyo na utulivu na matokeo yanayoweza kusababisha maafa. Juhudi zote zinapaswa kufanyika ili kuepusha matokeo haya mabaya, ikiwa ni pamoja na kurudi mara moja kwenye mazungumzo.
Alipoulizwa kama Guterres ana mpango wa kuzungumza na Putin kuhusu suala la New START au vita vya Ukraine, Dujarric amesema hana chochote cha kuwaambia waandishi wa habari kwa wakati huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma