

Lugha Nyingine
Kenya na Uganda zaanza mazungumzo ya kuanzisha kituo kimoja cha mpakani kwenye eneo lenye uhalifu
(CRI Online) Februari 22, 2023
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imesema Kenya na Uganda zimeanza mazungumzo ya kufungua kituo kimoja cha mpakani kwenye eneo la Lokiriama kaskazini magharibi mwa Kenya ili kuhimiza biashara na kulifungua zaidi eneo hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya Bw. Raymond Omollo amesema kituo hicho kitahimiza uvukaji wa watu na biashara, uwekezaji kwenye mtandao wa barabara za kuvuka mpaka na kuhimiza usalama na usimamizi kati ya nchi hizo mbili.
Eneo hilo la mpakani linakaliwa na jamii za waturkana na wapokot kwa upande wa Kenya, na wakaramajong kwa upande wa Uganda, jamii za wafugaji ambazo mara nyingi zimekuwa zikijihusisha na shughuli za uhalifu na kufanya eneo hilo kutokuwa salama.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma