Wanajeshi wa Somalia wawaua wapiganaji 42 wa al-Shabaab kusini mwa Somalia

(CRI Online) Februari 22, 2023

Jeshi la Somalia (SNA) limesema vikosi vyake vinavyoungwa mkono na vikosi vya ndani na vya kimataifa vimewaua wapiganaji 42 wa kundi la al-Shabaab katika operesheni iliyotekelezwa katika Wilaya ya Mahaday, Kusini mwa Somalia.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Utalii ya Somalia imesema katika taarifa yake kwamba vikosi vya jeshi vilikamata silaha wakati wa operesheni hiyo iliyolenga kuwafurusha makamanda wa al-Shabaab kutoka mafichoni mwao. Wizara hiyo imesema serikali ya Somalia imedhamiria kuwaondoa magaidi nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha