Rais Xi Jinping asisitiza utafiti wa kimsingi kwa ajili ya China kujitegemea katika sayansi na teknolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2023

BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa wito wa kuimarishwa kwa utafiti wa kimsingi ili kuimarisha na kuboresha uwezo wa kujitegemea na nguvu ya China katika sayansi na teknolojia.

Rais Xi alitoa wito huo alipoongoza semina elekezi ya tatu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC Jumanne.

Rais Xi amesema kuimarisha utafiti wa kimsingi ni hitaji la dharura kwa ajili ya kupata uwezo mkubwa wa kujitegemea zaidi katika sayansi na teknolojia, na ndiyo njia pekee ya kuwa nchi yenye nguvu katika sayansi na teknolojia duniani.

Amesema, kwa sasa, duru mpya ya mapinduzi ya kisayansi na mageuzi ya viwanda yanaendelea kwa kasi, ujumuishaji na mafungamano ya taaluma mbalimbali yanakua siku hadi siku, dhana ya utafiti wa kisayansi inapitia mabadiliko makubwa, ujumuishaji na mafungamano ya sayansi na teknolojia na maendeleo ya kiuchumi na kijamii unaongezeka, mzunguko wa matumizi ya utafiti wa kimsingi umefupishwa kwa udhahiri, na ushindani wa kimataifa katika utafiti wa kimsingi unasonga mbele.

Ameongeza kuwa, ili kuendana na ushindani wa kimataifa wa teknolojia na sayansi, kufikia uwezo wa kujitegemea zaidi, kuhimiza muundo mpya wa maendeleo, na kukuza maendeleo ya kiwango cha juu, kuna haja ya haraka ya kuimarisha utafiti wa kimsingi na kushughulikia teknolojia muhimu kutoka kwenye chanzo na kutoka chini.

Amesisitiza juhudi za kuimarisha muono wa mbali, kimkakati na mpangilio wa utaratibu wa utafiti wa kimsingi.

Pia ametoa wito wa kuimarishwa kwa upembuzi yakinifu na uteuzi na tathmini ya miradi mikuu ya utafiti wa kimsingi, kuheshimu kikamilifu ushauri wa wanasayansi, na kufahamu mwelekeo wa jumla wa kuanza mapema.

Rais Xi ameeleza kuwa ni muhimu kuimarisha nguvu za kimkakati za nchi katika sayansi na teknolojia; kuendeleza kwa kina utafiti wa kimsingi wa kimkakati, wa kipaumbele na soko kwa njia iliyopangwa; na kutoa jukumu kamili la maabara za kitaifa, taasisi za kitaifa za utafiti, vyuo vikuu vya juu vya utafiti na kampuni za mfano wa kuigwa za sayansi na teknolojia.

Rais Xi amesema, uwekezaji wa kifedha katika utafiti wa kimsingi unapaswa kuongezeka kwa hatua madhubuti, makampuni ya biashara yahamasishwe kuwekeza zaidi kupitia hatua kama vile kutoa nafuu za kodi, mchango kutoka kwa nguvu za kijamii unapaswa kuhimizwa, na ufanisi wa mfuko wa kitaifa wa sayansi ya asili na fedha zake za pamoja unapaswa kuboreshwa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha