Wasimamizi wa sekta ya afya wa Afrika wakutana nchini Kenya kuimarisha uwezo wa kupambana na magonjwa

(CRI Online) Februari 24, 2023

Maofisa wa afya kutoka zaidi ya nchi 30 wamekutana mjini Nairobi, Kenya ili kufanya mapitio ya namna ya kuimarisha uwezo wa mifumo ya afya ya nchi za Afrika.

Mwenyekiti wa Chama cha Mabaraza ya Afya ya Afrika Bw. Simon Nemutandani, amesema kwenye ufunguzi wa mkutano huo kuwa usalama wa wagonjwa unahitaji usimamizi mkali utakaopanua upatikanaji wa huduma bora za afya.

Amesema wasimamizi wa sekta ya Afya wa nchi za Afrika wanatakiwa kuunda mifumo inayoweza kukabiliana na changamoto za magonjwa ya mlipuko na majanga yanayotokana na hali ya hewa. Ameongeza kuwa wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga kubwa la COVID-19, serikali zinatakiwa kuongeza uwekezaji kwenye wahudumu wa afya na miundombinu ya afya.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha