Rais wa zamani wa Kenya awasili Nigeria kuongoza ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika

(CRI Online) Februari 24, 2023

Aliyekuwa Rais wa Kenya Bw. Uhuru Kenyatta amewasili Abuja, Nigeria kuongoza ujumbe wa watu 90 waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika (AUEOM) nchini humo.

Umoja wa Afrika umetoa taarifa ukisema ujumbe huo utafuatilia uchaguzi wa rais na wabunge unaopangwa kufanyika Februari 25.

Umoja huo umesema Bw. Kenyatta anatarajiwa kushirikiana na wadau wakuu kadhaa, akiwemo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, wagombea urais na inspekta jenerali wa polisi wa Nigeria.

Bw. Kenyatta pia atakutana na viongozi wa tume za waangalizi wa uchaguzi za kimataifa na jopo la mabalozi wa Afrika nchini Nigeria.

Jumla ya wagombea 18 wanagombea nafasi ya urais, huku idadi ya wapiga kura walioandikishwa ikiwa milioni 93.4 katika majimbo 36 na mji mkuu.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha