China yapanua mtandao wa usafirishaji na uchukuzi ili kuhimiza maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2023
China yapanua mtandao wa usafirishaji na uchukuzi ili kuhimiza maendeleo
Picha iliyopigwa Februari 4, 2023 ikionyesha daraja la kuvuka bahari la eneo la Ghuba ya Quanzhou, ambalo ni sehemu ya reli ya mwendo kasi ya kutoka Fuzhou hadi Xiamen, katika Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China. (Xinhua/Zhou Yi)

BEIJING - China imepata mafanikio makubwa katika kuboresha mtandao wake wa miundombinu ya uchukuzi na huduma za usafiri katika miaka mitano iliyopita, na itaendeleza ujenzi wa mfumo mpana wa usafirishaji katika siku zijazo, Wizara ya Uchukuzi ya China imesema, Alhamisi.

Waziri wa Uchukuzi wa China Li Xiaopeng amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, katika kipindi cha Mwaka 2018 hadi 2022, China ilijenga mitandao mikubwa zaidi ya reli ya mwendo kasi na barabara kuu kuliko nchi nyingine yoyote duniani, ikiwa ni pamoja na bandari zenye hadhi ya kimataifa.

Uwekezaji wa mali zisizohamishika katika mfumo wa usafirishaji na uchukuzi wa nchi umezidi Yuan trilioni 17 (kama dola trilioni 2.46 za Kimarekani) katika kipindi hicho,” Li amesema.

Kufikia mwisho wa Mwaka 2022, urefu wa jumla wa mtandao wa usafirishaji na uchukuzi wa China ulizidi kilomita milioni 6.

Jumla ya umbali wa uendeshaji wa reli wa China ilifikia kilomita 155,000, kati ya hizo reli za mwendo kasi zimefikia kilomita 42,000. China ilikuwa na jumla ya kilomita milioni 5.35 za barabara kuu kufikia mwisho wa Mwaka 2022, ambapo kati ya hizo barabara kuu zilichukua kilomita 177,000.

Takwimu kutoka wizara hiyo zinaonesha kuwa, kulikuwa na miundombinu ya usafirishaji na uchukuzi ipatayo 2,751 yenye ufanisi wa kuchukua tani 10,000 au zaidi kwa wastani kila mmoja na viwanja vya ndege 254 vilivyoidhinishwa kote nchini China kufikia mwisho wa mwaka jana.

Idadi ya abiria kwenye biashara ya usafiri nchini China ilifikia bilioni 5.59, mizigo iliyosafirishwa ilifikia tani bilioni 50.6, upitishaji wa bidhaa kwenye bandari kote China ulifikia tani bilioni 15.68, na upitishaji wa makontena ulizidi milioni 300.

Li amesema kuwa, China imekuwa ikihimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya sekta yake ya usafirishaji na uchukuzi, kuzidisha mabadiliko ya kijani na utoaji hewa chache ya kaboni, na kuboresha mazingira ya biashara yake.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha