Masoko mseto yachochea kwa kasi uchumi wa usiku wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2023

Mmiliki wa kibanda (wa kwanza kulia) akiuza bidhaa kwenye soko la mtaani lenye mvuto wa kiutamaduni huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Februari 19, 2023. (Xinhua/Guo Cheng)

HAIKOU - Usiku unapoingia, mtaa wa biashara wa Xixili huko Haikou, mji mkuu wa mkoa wa kisiwa wa Hainan, Kusini mwa China, unaingia kwenye pilikapilika nyingi za maisha.

Mchanganyiko wa mapambo yaliyotengenezwa kwa mikono na vitafunio hupamba mabanda mengi yaliyojengwa katika mtindo wa kambi kwenye magulio ya usiku, na kuvutia kwa wingi wakazi na watalii kutoka maeneo mbalimbali.

Wang Hongyu anajishughulisha na kutengeneza baga kwenye kibanda cha kuuza vitafunio. Huku pia akiendesha kampuni ya teknolojia ya mtandao wakati wa mchana, Wang huuza baga usiku kama upendeleo wake na kama kazi yake ya pili.

"Wamiliki wa vibanda hapa ama wanaona shughuli zao kama kazi ya kudumu au kazi ya muda mfupi ili kuongeza mapato," Wang amesema, huku akiongeza kuwa anaweza kupata mapato ya Yuan 10,000 (kama dola za Kimarekani 1,449) kwa usiku mmoja wenye shughuli nyingi.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, aina mpya za masoko ya usiku zimeibuka katika mji huo, na kuongeza matumizi katika ununuzi na kuingiza kasi katika ufufuaji wa uchumi kutoka kwenye hali ya kudorora wakati wa UVIKO-19.

"Tunafurahi kuona kuongezeka kwa masoko ya usiku hapa Haikou katika miaka ya hivi karibuni," mkazi Fei Luyuan wa Haikou amesema. "Yanakua ya vijana na yanafurahiwa na vijana zaidi."

Wang Ke, mkurugenzi wa idara ya utalii, utamaduni, redio, televisheni, na michezo ya Haikou, amesema serikali inaunga mkono kuibuka kwa masoko ya usiku ya aina mbalimbali, ambayo yanaweza kuchanganya na utamaduni mbalimbali na kukidhi matakwa ya watumiaji vijana.

Watalii wakitembelea soko la mtaani lenye mvuto wa kiutamaduni huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Februari 19, 2023. (Xinhua/Guo Cheng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha