Maoni ya Katuni: Marekani na Nchi za Magharibi Zinavyovumisha Kile Kinachoitwa "Mtego wa Madeni wa China"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2023
Maoni ya Katuni: Marekani na Nchi za Magharibi Zinavyovumisha Kile Kinachoitwa
Picha na Tan Xiguang

Hivi majuzi, wakati Shirika la Fedha la Kimataifa, Benki ya Dunia na India, ambayo ni mwenyekiti wa zamu wa Kundi la 20 (G20), walipofanya mkutano kwa njia ya video kujadili suala la deni la kimataifa, baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya Marekani na Nchi za Magharibi vilianza kuishutumu China bila sababu na kupigia debe kile kinachoitwa, "Mtego wa madeni wa China".

Katika muda mfupi uliopita, maofisa waandamizi wa Marekani walifanya ziara katika nchi kadhaa za Afrika kwa mfululizo, ambapo walihusisha mzigo wa madeni wa nchi za Afrika na China.

Kwa hakika, Marekani na Nchi za Magharibi ndio watengenezaji wa "mtego wa madeni" wa nchi zinazoendelea. Ripoti nyingi kutoka kwa taasisi za kimataifa na nyanja za utafiti wa kitaalamu zinaonyesha kuwa chanzo cha deni la nje la nchi za Afrika ni dhamana zinazoshikiliwa na wakopeshaji wa kibinafsi kutoka Nchi za Magharibi.

Kuilaumu China kwa tatizo la madeni si chochote zaidi ya Marekani na Nchi za Magharibi kujaribu kuwachanganya wananchi na kukwepa wajibu wao. Ujanja huu wa kupiga kelele za "zuia mwizi" hautafanikiwa.

 

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha