Mamlaka ya hali ya hewa ya Rwanda yatabiri mvua kubwa katika miezi ijayo

(CRI Online) Februari 27, 2023

Mvua kubwa zinazoanzia mwezi Machi hadi Mei zinaweza kuleta majanga makubwa katika sehemu mbalimbali za Rwanda.

Kwenye utabiri wake mpya Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Rwanda imeonya kuwa mvua kubwa za ujazo wa milimita kati ya 500 na 600 katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo zinaweza kuleta majanga kama vile mafuriko, maporomoko ya udongo, upepo mkali na majanga mengine yanayohusiana na hali ya hewa. Hata hivyo mamlaka pia imetabiri mvua nyepesi katika sehemu za kusini mwa nchi na sehemu nyingi za Kigali kuanzia Mei 20 hadi 25.

Mamlaka vilevile imeshauri umma hasa wakulima kutumia utabiri huo kuweka mipango yao ya upandaji mazao, mavuno na shughuli za usimamizi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha