WHO yaitaka Afrika kukabiliana haraka na ugonjwa wa kipindupindu

(CRI Online) Februari 27, 2023
WHO yaitaka Afrika kukabiliana haraka na ugonjwa wa kipindupindu

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa taarifa likisema Afrika inashuhudia ongezeko kubwa la wagonjwa wa kipindupindu kufuatia wimbi kubwa la ugonjwa huo duniani, ambapo idadi ya wagonjwa waliorikodiwa barani humo katika mwezi wa kwanza mwaka 2023 pekee tayari imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 ya idadi ya jumla ya mwaka mzima wa 2022.

Kwa mujibu wa Ofisi ya WHO kanda ya Afrika, iliyopo Brazzaville, nchini Jamhuri ya Congo, makadirio ya wagonjwa 26,000 na vifo 660 yameripotiwa hadi kufikia Januari 29 katika nchi kumi za Afrika zinazokabiliwa na mlipuko tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Karibu wagonjwa 80,000 na vifo 1,863 vimerikodiwa katika nchi 15 zilizoathirika katika mwaka 2022, huku wagonjwa 141,467 na vifo 4,094 vikiandikishwa mwaka 2021.

WHO imeonya kuwa kama wimbi hili la ugonjwa linaloongezeka kwa kasi litaendelea, maambukizi katika mwaka huu yanaweza kuzidi idadi ya wagonjwa iliyorikodiwa mwaka 2021, ambao ni mbaya kwa kipindupindu katika Afrika karibu kwa mwongo mzima. Wastani wa idadi ya vifo kwa hivi sasa ni karibu asilimia 3, ambayo imezidi asilimia 2.3 ya mwaka 2022, huku kiwango kinachokubalika cha ongezeko ni chini ya asilimia 1.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha