UM wasema watoto na wanawake takriban milioni 4 wana utapiamlo mkali Sudan

(CRI Online) Februari 27, 2023
UM wasema watoto na wanawake takriban milioni 4 wana utapiamlo mkali Sudan

Umoja wa Mataifa umesema watoto na wanawake takriban milioni 4 wanasumbuliwa na utapiamlo mkali nchini Sudan.

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) nchini Sudan jana Jumapili ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema, watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha takriban milioni 4 wanakadiriwa kuwa na utapiamlo mkali na kuhitaji huduma za lishe ili kuokoa maisha yao katika mwaka 2023, ambapo watu laki 6.11 kati yao wana utapiamlo mbaya zaidi.

Ofisi ya OCHA ilisema hali ya utapiamlo mkali inatokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ulaji duni wa lishe, hali mbaya ya magonjwa ya kuambukiza, njia isiyo sahihi ya kutunza na kunyonyesha watoto, na hali mbaya ya afya, maji, na usafi. Iliongeza kuwa hali mbaya ya kiuchumi, mfumko wa bei na kukimbia makazi pia zimechangia utapiamlo mkali katika mwaka 2022, hali ambayo inaweza kuendelea katika mwaka 2023.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha