“Kupanda mikomamanga, kupata maua ya mshikamano ”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2023

Maimaiti Yibureyimu Maimaitiming ni katibu wa Kamati ya chama ya Kijiji cha Bashiyujimai cha Wilaya ya Cele ya Eneo la Hotan la Mkoa wa Xinjiang. Hapa kuna hadithi kuhusu makomamanga.

Februari 20, Maimaiti Yibureyimu Maimaitiming (katikati) alitembelea nyumbani kwa wanakijiji. (Picha na Ding Lei/Xinhua)

Ilikuwa Machi 10, 2017. Katibu Mkuu Xi Jinping alihudhuria mjadala wa ujumbe wa Xinjiang kwenye Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 12. Baada ya Maimaiti Yibureyimu kutoa hotuba ya utekelezaji wa sera ya kuwanufaisha watu , alimwambia katibu mkuu: "Nataka kuripoti jambo moja zaidi."

“Sema tu.” katibu Mkuu alimwambia .

“Hivi majuzi ulijibu barua kwa familia ya Bwana Kurban, walifurahi sana na kuniomba nikuletee picha kadhaa , pia walisema kwamba watakumbuka wema wa chama kama Katibu Mkuu ulivyosema kwenye barua, na watakuwa ubavuni mwa Chama kama mbegu za komamanga zinavyoshikamana."

Katibu Mkuu alisema kwa tabasamu: “kweli ni familia yenye watu wengi sana.”

Katibu Mkuu aliuliza: “kwenye familia yako, kuna mtu amekuwa msaidizi wa mtu mwingine anayehitaji msaada ? ?

“Ndiyo ndiyo.” Maimaiti Yibureyimu alijibu kwa maneno mengi.

Baada ya kusikiliza jibu lake, Katibu Mkuu alisema: “shughuli za kuwa msaidizi wa mtu anayehitaji msaada wa kuondokana na umaskini zikifanyika kwa umakini na kwa vitendo vya halisi, zitakuwa na umuhimu kwa umoja wa makabila.”

Februari 20, Maimaiti Yibureyimu Maimaitiming akieleza hatua za kunufaisha watu kwa wanakijiji. (Picha na Ding Lei/Xinhua)

Baada ya kurejea Xinjiang, Maimaiti Yibureyimu aliwaambia wanakijiji katibu mkuu kutilia maanani maendeleo ya Xinjiang na kujali maisha ya watu; aliingia shuleni na kuwaambia watoto maana ya "mbegu za komamanga" "; alianzisha ofisi ya "Usuluhisho" ili kutatua matatizo na migongano ya watu. Katika miaka michache iliyopita, ameona uhusiano kati ya wanakijiji umekuwa wa maafikiano zaidi , na kazi za maofisa wa kijiji zimeendelea vizuri siku hadi siku .

Maimaiti Yibureyimu aliwaambia wanakijiji hao: "Katibu Mkuu Xi Jinping amesisitiza mara kwa mara kwamba 'umoja wa kitaifa ndio msingi wa maendeleo', kama tutakuwa na hali ya utulivu na mshikamano, ndipo shughuli za uzalishaji na maisha zitafanyika kwa utaratibu. Ni lazima sote tufanye kazi pamoja kwa ushirikiano, kupanda mikomamanga,ili kujionea maua ya umoja yachanue na kupata matunda ya furaha!"

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha