Ripoti ya Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani yaonyesha China bado ni nchi yenye nguvu ya kuvutia uwekezaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2023
Ripoti ya Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani yaonyesha China bado ni nchi yenye nguvu ya kuvutia uwekezaji
Picha iliyopigwa Mei 7, 2019 ikionyesha magari yakiwa kwenye Kiwanda cha kuunda magari cha Tiexi cha BMW Brilliance (BBA) huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua/Yang Qing)

GUANGZHOU – Ripoti iliyotolewa Jumatatu na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani la Huanan unaonyesha kuwa China bado inachukuliwa kuwa moja ya maeneo ya kuvutia zaidi kwa uwekezaji huku kampuni nyingi zikipanga kuwekeza tena nchini China mwaka huu.

Waraka wa mwaka wa shirikisho hilo kuhusu mazingira ya biashara ya China unaonekana kama dirisha la kutazama mazingira ya biashara ya China kupitia macho ya kampuni zinazowekezwa na mataifa ya kigeni.

Waraka huo unatokana na utafiti unaohusisha zaidi ya kampuni 200 kuanzia Septemba hadi Desemba Mwaka 2022. Miongoni mwa kampuni zilizofanyiwa utafiti, asilimia 40 ni kampuni zinazomilikiwa na wageni, na karibu asilimia 20 ni kampuni wakilishi za makampuni ya kigeni na zile zinzomilikiwa kwa ubia.

Waraka huo umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya kampuni zilizoshiriki kwenye utafiti huo zinaichagua China kuwa mojawapo ya maeneo muhimu ya uwekezaji.

Likiwa na zaidi ya wanachama 2,300, shirikisho hilo linatoa usaidizi kwa makampuni ya Marekani na kimataifa yanayofanya biashara kwenye eneo la Kusini mwa China.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha