Kamati Kuu ya CPC yafanya mkutano wa mashauriano juu ya mpango wa mageuzi ya vyombo vya Chama na serikali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2023

BEIJING - Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wa mashauriano Jumanne ili kusikiliza maoni na kujulisha vyama vya kisiasa visivyo vya CPC, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC) na watu wasio wa chama chochote katika mpango wa mageuzi ya vyombo vya Chama na serikali.

Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), aliongoza mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.

Wajumbe waliohudhuria walijulishwa juu ya mpango wa kuimarisha mageuzi ya vyombo vya Chama na serikali. Pia wamearifiwa kuhusu orodha ya maofisa viongozi wanaopendekezwa wa idara za serikali ambayo itawasilishwa kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China ili kuthibitishwa. Wamearifiwa pia juu ya orodha ya maofisa viongozi waliopendekezwa wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China ambayo itawasilishwa kwenye mkutano ujao wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa ili kuthibitishwa.

Wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi walihudhuria kwenye mkutano huo.

Rais Xi amesema Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliweka mipango mikubwa juu ya kuimarisha mageuzi ya vyombo vya chama na serikali, kwa maelekezo ya wazi katika maeneo kadhaa. Haya ni pamoja na kuimarisha mageuzi ya mfumo na muundo wa mambo ya fedha na kukamilisha mfumo wa uongozi wa pamoja wa Kamati Kuu ya Chama katika kazi za sayansi na teknolojia.

Xi anatumai kuwa vyama vya kisiasa visivyo vya CPC, Shirikisho la viwanda na biashara na watu wasio wa chama chochote wataunga mkono kwa dhati mageuzi hayo ili kuhakikisha majukumu yote yanakamilishwa kwenye mikutano hiyo miwili ijayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha