

Lugha Nyingine
China yatangaza mpango kabambe wa kupanua kituo chake cha anga ya juu
![]() |
Picha hii ya skrini iliyopigwa kwenye Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Februari 9, 2023 ikionyesha mwanaanga wa Chombo cha Anga ya Juu cha Shenzhou-15 Fei Junlong akifanya shughuli za ziada (EVAs) nje ya moduli ya maabara ya Wentian ya kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Liu Fang) |
BEIJING – Kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye Jumba la Makumbusho ya Kitaifa la China, imetangazwa kuwa China inapanga mpango kabambe wa kupanua kituo chake cha anga ya juu katika obiti ya karibu na Dunia kwa kuzindua moduli mpya ambayo itatia nanga pamoja na muundo uliopo na kuunda umbo la mchanganyiko la kupishana.
Kwenye maonyesho hayo ambayo yanaangazia mafanikio katika mpango wa anga ya juu wa China katika miaka 30 iliyopitra, Shirika la Anga za Juu la China (CMSA) limetangaza hadharani mipango yake ya ufuatiliaji baada ya mkusanyiko na ujenzi wa muundo wa umbo la T wa kituo hicho mwaka jana.
Shirika hilo limesema, moduli mpya, ambayo itafanya kazi kama kabini ya nodi, itakuwa na maeneo mengi ya kutua kwa vyombo kama moduli ya msingi ya Tianhe, ikiruhusu kituo cha anga ya juu kushughulikia vyombo vingi vya anga ya juu.
CMSA imeongeza kuwa China inapanga kupanua ufanisi wa kazi katika obiti ya kituo chake cha anga ya juu kwa kutekeleza mahuisho ya teknolojia mpya na uboreshaji.
Maonyesho hayo pia yameonyesha maendeleo ya China ya chombo kipya cha kizazi kipya kinachoweza kutumika tena karibu na Dunia chenye uwezo wa kubeba wanaanga wanne hadi saba kwenye anga ya juu na kurudisha zaidi ya kilo 700 za mizigo duniani. Chombo kilichopo sasa kinaweza kuwarusha wanaanga watatu kwenye anga ya juu na kubeba kilo 50 za mizigo.
CMSA imeeleza kuwa katika miaka ijayo, zaidi ya maombi 1,000 katika miradi 65 yatatekelezwa kwenye kituo cha anga ya juu. Jitihada hizi zinalenga kuendeleza teknolojia muhimu katika utayarishaji wa nyenzo maalum, kuhusu elumu ya matibabu ya utafiti wa seli shina na njia za kujizalisha upya na kufufuka kwake, mifumo ya usahihi wa hali ya juu ya masafa ya muda, na kipimo cha usahihi wa quantum.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma