

Lugha Nyingine
Matokeo ya uchunguzi kuhusu Mikutano Miwili 2023 ya China yaonesha watu wanafuatilia zaidi masuala ya elimu na vipaji, huduma za jamii na kupambana na ufisadi
Kuanzia tarehe 1 hadi 27, Februari, tovuti ya Gazeti la Umma ilifanya uchunguzi kuhusu mikutano miwili 2023 ya China, yaani mkutano wa Bunge la Umma la China na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China. Uchunguzi huo ni wa 22 kufanywa na tovuti hiyo, na umevutia watu zaidi ya milioni 5.81 kushiriki.
Kutokana na matokeo ya kura zilizopigwa na watumiaji wa mtandao, “elimu na vipaji”, “huduma za jamii”, “kupambana na ufisadi ”, “ustawishaji wa vijiji”, “kipaumbile cha ajira”, “matibabu na usafi ”, “utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria”, “usimamizi wa jamii”, “kupanua mahitaji ndani na kuhimiza matumizi” na “mchakato mzima wa demokrasia ya umma” yamechaguliwa kuwa masuala makumi ya juu yanayofuatiliwa zaidi.
Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa, suala la “elimu na vipaji” linafuatiliwa zaidi na watumiaji wa mtandao. Kwa mara ya kwanza Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliofanyika mwaka jana umeweka “elimu ya kidijitali” kwenye ripoti yake.
Katika uchunguzi wa mara zote kuhusu mikutano mikuu miwili ya China uliofanywa na tovuti ya Gazeti la Umma, hii ni mara ya 19 kwa “huduma za jamii” kuchaguliwa kuwa moja ya masuala ya juu yanayofuatiliwa zaidi.
Katika uchunguzi wa mwaka huu, masuala ya “kupambana na ufisadi ” yamefuatiliwa tena na zaidi na watumiaji wa mtandao. Watumiaji wa mtandao wametoa maoni wakitumai kuongezwa kwa uwazi kwenye mambo ya utawala, ili kutoa mazingira kwa umati wa watu kufanya usimamizi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma