

Lugha Nyingine
Msemaji: China sio mdai mkubwa zaidi barani Afrika
(CRI Online) Machi 04, 2023
(Picha inatoka CRI.)
Msemaji wa kikao cha kwanza cha Bunge la 14 la Umma la China, Wang Chao amesema China sio mdai mkubwa zaidi barani Afrika kwani takwimu kutoka Benki ya Dunia zinaonesha kuwa karibu robo tatu ya deni la nje la Afrika linatoka kwenye taasisi za fedha za kimataifa na wakopeshaji wa kibiashara.
Akiongea na waandishi wa habari siku moja kabla ya ufunguzi wa kikao hicho cha mwaka, Bw. Wang amesema China siku zote imekuwa ikijitolea kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza mzigo wa madeni na kupinga madai kwamba China inatengeneza kile kinachoitwa "mitego ya madeni" katika Afrika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma