Mkutano wa Bunge la Umma la China wafunguliwa Beijing

(CRI Online) Machi 05, 2023

(Picha inatoka CRI.)

Mkutano wa kwanza wa awamu ya 14 ya Bunge la Umma la China umefunguliwa leo Jumapili hapa Beijing, na kuhudhuriwa na viongozi wa China akiwemo rais Xi Jinping. Waziri Mkuu Bw. Li Keqiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali.

Bw. Li amesema kwenye ripoti ya kazi ya serikali kwamba mwaka 2022 ulikuwa ni mwaka muhimu katika historia ya Chama cha Kikomunisti cha China na taifa. Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulifanyika kwa mafanikio, na kuweka mipango kuhusu ujenzi wa nchi ya ujamaa wa kisasa kwa pande zote.

Bw. Li pia amesema ili kukabiliana na mazingira yenye utatanishi ya kimataifa, na kazi ngumu ya mageuzi, na kuimarisha maendeleo na utulivu nchini, Kamati Kuu ya Chama ikiongozwa na rais Xi Jinping imewaongoza watu wa makabila yote kote nchini, kukabiliana na changamoto na kutekeleza kikamilifu kazi ya kuzuia magonjwa, kutuliza hali ya uchumi na kuhakikisha maendeleo kwa usalama, kuongeza nguvu ya usimamizi wa hali ya jumla, na uchumi umekuwa ukiendelea vizuri, ubora wa maendeleo umeinuka kwa kasi, na utulivu wa hali ya kijamii umedumishwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha