Kitoweo cha Guangping Zengzhou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2023

Guangping Zengzhou ni kitoweo kimoja kilichoanza kujulikana katika kipindi cha Mfalme Xianfeng wa Enzi ya Qing, na kimekuwa na historia ya miaka 200, ambapo kinapikwa kwa nyama za mguu wa mbele wa nguruwe. Kinatumia nyama za miguu ya mbele ya nguruwe, mnofu, na viungo vya siri. Ladha yake na harufu nzuri imerithi ile ya zaidi ya miaka mia moja. Kila ifikapo Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kitoweo hiki kitamu ni lazima kipikwe kwa ajili ya kuwakirimu jamaa na marafiki.

Hatua za kupika: Kwanza unatakiwa kuchuna ngozi na kuondoa mifupa. Kisha kuhifadhi mnofu wake na kuukata vipande vidogovidogo, halafu ondoa manyoya kwenye ngozi na kuyaweka kando.

Baada ya hapo saga viungo zaidi ya kumi kama vile anise, fenesi na karafuu hadi viwe unga kwa kiasi kinachofaa,kisha changanya pamoja na nyama na kuziloweka kwa saa 6.

Hatimaye, baada ya kuzishona, mguu wa nguruwe utaonekana kama wa awali, kisha unafungwa kwa kitambaa na nyuzi za pamba ili kuhakikisha umbo lake, na baada ya kuchemshwa kwenye mchuzi wa supu kwa saa 12, chakula hicho kitamu kitakuwa tayari kimeiva, na tayari kuliwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha