Wizara ya Kilimo ya China: kazi ya uandaaji wa mbolea kwa ajili ya msimu wa kupanda inaendelea vizuri

(CRI Online) Machi 07, 2023

Takwimu zilizotolewa na wizara ya kilimo na vijiji ya China zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Februari, usambazaji wa mbolea kwa ajili ya msimu wa upandaji wa mwaka huu katika mikoa, miji na wilaya umekuwa kasi zaidi kuliko wakati kama huo wa mwaka jana.

Usambazaji wa mbolea katika mikoa mikubwa ya uzalishaji wa nafaka kama vile Liaoning, Anhui, Shandong, Hunan umemalizika kwa zaidi ya asilimia 80. Kwa jumla utoaji wa mbolea za aina muhimu unaweza kukidhi mahitaji ya msimu wa upandaji wa mwaka huu nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha