Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” latandika njia pana kwa ajili ya kupata maendeleo kwa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2023

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang akijibu maswali kwenye mkutano na waandishi wa habari kando ya mikutano miwili ya mwaka tarehe 7, Machi hapa Beijing, China. (Picha inatoka Xinhua.)

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang leo kwenye mkutano na waandishi wa habari kando ya mikutano miwili ya mwaka alipojibu maswali kuhusu kuna uhusiano wa ushindani au la kati ya Pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Mpango wa Marekani na Ulaya wa ujenzi wa miundombinu duniani alisema, “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni pendekezo la kufuata hali halisi na kufungua mlango, ambalo linafuata kanuni za kufanya mashauriano na ujenzi kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja. Kuhusu pendekezo la nchi nyingine, kama nchi hizo haziweki wigo la kiitikadi na bila vitu vyao binafasi vya kijioglafia, tunafurahi kuona lipate mafanikio yake.

Qin Gang amesema, mpaka sasa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limevutia zaidi ya robo tatu ya nchi duniani na mashirika 32 ya kimataifa. Miaka 10 imepita tangu pendekezo hilo litolewe, nalo limevutia uwekezaji wa dola za Marekani karibu trilioni moja katika zaidi ya miradi 3000, ambapo ujenzi wa miradi hiyo umeongeza nafasi za ajira laki 4.2 kwa nchi zilizoko kwenye ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuwasaidia watu karibu milioni 40 kuondokana na umaskini. Mwaka huu, China itatumia fursa ya kuandaa mkutano wa 3 wa wakuu wa ushirikiano wa kimataifa kwa kushirikiana na pande mbalimbali katika kuhimiza ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kupata matunda kemkem zaidi.

Qin Gang amesema, kofia ya ati “mtego wa deni” kabisa haifai kuvalishwa kwa China. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, katika madeni yanayodaiwa ya nchi zinazoendelea, madeni yanayodaiwa na taasisi za mambo ya fedha na benki za biashara yanachukua asilimia 80. Hasa tokea mwaka jana, Marekani iliongeza faida ya akiba benkini kwa kasi zaidi kuliko hapo kabla, ikasababisha mitaji ya nchi mbalimbali kuhamishwa nje mfululizo na kuzifanya nchi husika kubeba madeni mazito zaidi.

Qin Gang amesema, siku zote China inafanya juhudi za kuzisaidia nchi husika kupunguza taabu. Upande wa China ukiwa kwa msimamo wa kiujenzi utaendelea kushiriki katika utatuzi wa matatizo ya madeni ya kimataifa, na pia tunatoa wito wa kuzitaka pande nyingine mbalimbali zichukue vitendo vya pamoja, na zibebe wajibu kwa usawa. Pande mbalimbali zikikaa pamoja kwa kufanya mashauriano, hakika zitapata njia za ufumbuzi zaidi kuliko matatizo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha