Mpango wa Mageuzi ya Vyombo vya Baraza la Serikali la China wapitishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2023

Kikao cha tatu cha mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China kikifanika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma tarehe 10, Machi, 2023. (PIcha inatoka Xinhua)

Tarehe 10, Machi, Bunge la Umma la China limepitisha mpango wa mageuzi ya vyombo vya baraza la serikali la China.

Mpango huo wa mageuzi uliwasilishwa tarehe 7, Machi kwenye kikao cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China kwa kuthibitishwa. Mambo muhimu kwenye mageuzi hayo ni pamoja na kuunda upya Wizara ya Sayansi na Teknolojia, kuunda Idara Kuu ya Ukaguzi na Usimamizi wa Mambo ya Fedha, kuunda Idara ya Kitaifa ya Takwimu, kukamilisha majukumu na wajibu wa Wizara ya Kilimo na Vijiji, kukamilisha mfumo wa kazi kuhusu wazee, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa hakimiliki ya ubunifu, kubadilisha Idara ya Kitaifa ya Kupokea Malalamiko kuwa chombo chini ya Baraza la Serikali la China, na kupunguza watumishi kwenye vyombo vya serikali kuu.

Mageuzi ya vyombo vya baraza la serikali la China ni hatua muhimu ya kuongeza uwezo wa utawala na kuinua ufanisi katika mazingira ya dunia yenye utatanishi. Yanaweka mkazo katika kuondoa matatizo magumu yanayofuatiliwa na watu, na yataleta ushawishi mkubwa kwa maendeleo ya jamii na uchumi ya China.

Katika muongo ulipotia, China imefanya marekebisho ya kimfumo na kikamilifu juu ya kazi na majukumu na wajibu wa vyombo vya Chama na serikali kuu, marekebisho hayo yameinua juu kiwango cha usasa cha mfumo na uwezo wa utawala wa nchi ya China.

Hata hivyo, kwa kukabiliwa na kipindi kipya cha maendeleo, mazingira mapya ya maendeleo na fursa mpya za kimkakati za maendeleo, kuna haja ya lazima kuendeleza kwa kina mageuzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha