Kuacha njia na kupinduka kwa treni kwaonyesha sumu kwenye siasa za Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2023

(Katuni na Ma Hongliang.)

Hivi majuzi, treni iliyobeba vitu hatarishi iliacha njia na kupinduka kwenye eneo la Palestina Mashariki, Ohio, Marekani, na kumwaga kiasi kikubwa cha kemikali zenye sumu angani, ardhini na majini na kusababisha uharibifu mkubwa kwa mazingira ya eneo hilo.

Takwimu zilizotolewa na Idara ya Maliasili ya Ohio Februari 23 zinakadiria kuwa ajali hiyo ilisababisha takriban wanyama wa majini 44,000 kuuawa. Idara hiyo pia inakadiria kuwa takriban viumbe maji aina ya minnows 38,222 na viumbe wengine wa majini wapatao 5,500, ikiwa ni pamoja na samaki wadogo, amfibia, kamba, na viumbe wengine wakubwa wenye uti wa mgongo wameuawa katika eneo hilo la ajali ya treni ya mizigo lenye ukubwa wa kilomita 8.

Wakaazi wa eneo hilo wamelalamika kuwa wamekuwa wakikohoa kila siku na kuwa na vipele usoni na mikononi kufuatia ajali hiyo.

Badala ya kutatua matatizo haya ya dharura, vyama viwili vikuu vya kisiasa nchini Marekani vya Republican na Democrats vimeelekeza nguvu zao katika kushambuliana tena. Chama cha Republican kinamkosoa Rais wa Marekani Joe Biden kwa kutokwenda eneo la Palestina Mashariki badala yake kutembelea na kuongeza uungaji mkono wa kijeshi kwa Ukraine.

Wakati wa ziara yake katika eneo hilo la Palestina Mashariki, Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alishutumu serikali na uongozi wa Rais Biden kwa "kutojali na usaliti" katika kukabiliana na ajali hiyo ya kuacha njia na kupinduka kwa treni ya mizigo iliyokuwa imebeba kemikali hatarishi.

Waziri wa Uchukuzi wa Marekani Pete Buttigieg, ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Democrats, naye alimlenga na kumshutumu Trump kwa kusema kwamba anapaswa "kuonyesha uungaji mkono kwa kubadilisha hali ya kutokuwepo kwa usimamzi iliyotokea chini ya uangaizi wake." wakati akiwa rais wa kipindi hicho.

"Kila wakati maafa yanapotokea katika nchi ya Marekani liyogawanyika, siasa zenye sumu haziko nyuma," makala iliyochapishwa kwenye tovuti ya Shirika la Utangazaji la CNN imesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha