Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kuchagua viongozi wapya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2023

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akiongoza kikao cha tatu cha Tume Tendaji ya Wenyeviti ya mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPCCC) kilichofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 9, 2023. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - Orodha ya wagombea wa uongozi mpya wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo kikuu cha ushauri wa kisiasa cha China, imeidhinishwa Alhamisi.

Ikiwa imepitishwa kwenye Tume Tendaji ya Wenyeviti ya mkutano wa kwanza unaoendelea wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa kwenye mkutano Alhamisi alasiri, orodha hiyo ya majina ya viongozi wapya itawasilishwa kwenye mkutano wa wajumbe wote kwa ajili ya kupigiwa kura ya mwisho leo Ijumaa alasiri.

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameongoza kikao hicho cha Tume Tendaji ya Wenyeviti.

Orodha ya majina ya viongozi waliopendekezwa inajumuisha nafasi za mwenyekiti, naibu mwenyeviti, katibu mkuu na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa.

Utaratibu wa uchaguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa ulipitishwa katika mkutano huo.

Kikao hicho pia kimepitisha rasimu ya azimio la ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa , rasimu ya azimio la ripoti ya kazi ya mapendekezo kutoka kwa wajumbe washauri wa kisiasa, rasimu ya marekebisho ya katiba ya Baraza la mashauriano ya kisiasa, rasimu ya ripoti ya kuthibitisha mapendekezo, na rasimu ya azimio la kisiasa la mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa.

Imeamuliwa kuwa rasimu zote zitawasilishwa kwa kupitishwa kwenye kikao cha kufunga mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa.

Kikao cha pili cha Tume Tendaji ya Wenyeviti, pamoja na kikao cha video cha mkutano wa CPPCC, pia kilifanyika Alhamisi.

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ni mfumo muhimu wa ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa CPC.

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akiongoza kikao cha pili cha Tume Tendaji ya Wenyeviti ya mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPCCC) kilichofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 9, 2023. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha