Kiongozi Mwandamizi wa CPC ashiriki kwenye majadiliano ya ujumbe wa Taiwan kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la 14 la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2023

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Taiwan kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) unaofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 9, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Alhamisi alishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Taiwan kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC).

Wang amehimiza kutekeleza kikamilifu mipango na maagizo elekezi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, kutekeleza sera ya jumla ya Chama kwa ajili ya kusuluhisha suala la Taiwan katika zama mpya, kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na Makubaliano ya Mwaka 1992, na kufanya juhudi za kuweka maendeleo ya uhusiano kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan katika mwelekeo sahihi.

Amesisitiza kutekeleza bila kuyumbayumba kwa matarajio ya Muungano wa Amani wa Taifa la China, kuendeleza mabadilishano, ushirikiano na maendeleo jumuishi katika Mlango-Bahari wa Taiwan, kupinga shughuli za watu wanaotaka “Taiwan Kujitenga”, na kupinga kuingiliwa na nchi za nje.

Wang pia ametoa wito wa kuungana mkono na ndugu wa Taiwan ili kufikia Muungano kikamilifu wa Taifa la China na Ustawi mkubwa wa Taifa la China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha