Bunge la Umma la 14 la China lachagua viongozi wapya wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2023
Bunge la Umma la 14 la China lachagua viongozi wapya wa China
Xi Jinping aliyechaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Watu wa China (PRC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akila kiapo cha utii kwa Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China katika hafla iliyofanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 10, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

Xi Jinping amechaguliwa kuwa Rais wa China siku ya Ijumaa kwenye mkutano wa kwanza unaoendelea wa Bunge la Umma la 14 la China, akiiongoza nchi hiyo yenye watu zaidi ya Bilioni 1.4 kwenye safari mpya ya kuelekea maendeleo ya kisasa.

Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi (CMC) ya Jamhuri ya Watu wa China (PRC) kwa kupigiwa kura zote za ndiyo.

Jumla ya wajumbe 2,952 walihudhuria kwenye kikao cha tatu cha Mkutano wa Kwanza wa wajumbe wote wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) siku ya Ijumaa asubuhi, kutumia haki zao za msingi za kikatiba kuchagua viongozi wapya wa Serikali ya China.

Pia siku hiyo ya Ijumaa, wajumbe hao walimchagua Zhao Leji kuwa Spika wa Bunge la Umma la 14 la China, na Han Zheng amechaguliwa kuwa Naibu Rais wa China.

Jumla ya watu 14 wamechaguliwa kuwa manaibu wenyeviti na makatibu wakuu wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la 14 la China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha