Saudi Arabia na Iran zasaini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia, kufungua ubalozi katika pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2023

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC akiongoza mkutano wa kufungwa kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa Saudi Arabia na Iran hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 10, 2023. (Xinhua/Luo Xiaoguang)

BEIJING – Kama ilivyotangazwa na China, Saudi Arabia na Iran siku ya Ijumaa, nchi mbili hizo za Saudi Arabia na Iran zimefikia makubaliano ambayo yanahusisha makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na kufungua tena ubalozi na ujumbe wa kidiplomasia kati ya pande hizo mbili ndani ya miezi miwili.

Musaad bin Mohammed Al-Aiban, Waziri wa Nchi, Mjumbe wa Baraza la Mawaziri na Mshauri wa Usalama wa Taifa la Saudi Arabia aliongoza ujumbe wa Saudi Arabia, na Admiral Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, aliongoza ujumbe wa Iran kwenye mazungumzo yaliyofanyika Beijing kuanzia Machi 6-10, taarifa ya pande tatu za China, Saudi Arabia na Iran imesema.

Taarifa hiyo imesema, Saudi Arabia na Iran zimefanya majadiliano ili kusuluhisha tofauti zao kupitia njia za mazungumzo na kidiplomasia, ili kuendana na kufuata malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC), na kufuata kanuni na mazoea ya utendaji wa kimataifa .

Taarifa hiyo imesema kuwa, nchi zote mbili za Saudi Arabia na Iran zimetoa pongezi na shukrani kwa Iraq na Oman kwa kuandaa duru nyingi za mazungumzo kati ya Mwaka 2021 na 2022, na kwa viongozi wa China na Serikali ya China kwa kuwa mwenyeji, kuunga mkono na kuchangia mafanikio ya mazungumzo hayo. 

Wang Yi (Kati), Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akihudhuria mkutano wa kufungwa kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa Saudi Arabia ukiongozwa na Musaad bin Mohammed Al-Aiban (kushoto), Waziri wa Nchi, Mjumbe wa Baraza la Mawaziri na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Saudi Arabia, na ujumbe wa Iran ukiongozwa na Admiral Ali Shamkhani (Kulia), Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 10, 2023. Wang Yi aliongoza mkutnao huo hapa siku ya Ijumaa. (Xinhua/Luo Xiaoguang)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha