Wanaanga wa China walioko kwenye chombo cha Shenzhou-15 watarudi duniani mwezi Juni

(CRI Online) Machi 13, 2023

Shirika la vyombo vya anga ya juu vya kubeba binadamu la China CMSA limetangaza kuwa, wanaanga walioko kwenye chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15 watarudi duniani mwezi Juni.

Kwa sasa wanaanga hao wanaendelea katika hali nzuri na kituo cha anga ya juu cha China kinaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Imefahamika pia kuwa mwaka huu China itarusha vyombo vitatu kwenye anga ya juu, ikiwa ni pamoja na chombo cha Tianzhou-16 cha kubeba mizigo, na Shenzhou-16 na 17 vitakavyobeba wanaanga. Tayari wanaanga watakaokuwa kwenye vyombo hivyo tayari wamechaguliwa, na sasa wanaendelea na mafunzo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha