Bunge la Umma la 14 la China laidhinisha baraza jipya la serikali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2023

Kikao cha tano cha Mkutano wa Kwanza wa wajumbe wote wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) ukifanyika kwenye Jumba la Mikutano la Umma hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 12, 2023. (Xinhua/Li Xin)

BEIJING - Bunge la Umma la 14 la China Jumapili liliamua safu mpya ya Baraza la Serikali la China, katika mkutano wake wa mwaka ambao umefungwa leo.

Baada ya kuteuliwa na Waziri Mkuu Li Qiang, manaibu mawaziri wakuu, makansela wa serikali ya China, mawaziri, mkuu wa benki kuu, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na Katibu Mkuu wa Baraza la Serikali la China wameidhinishwa na wajumbe katika kikao cha tano cha Mkutano wa Kwanza wa wajumbe wote wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC).

Rais Xi Jinping wa China alitia saini amri ya rais kuwateua maofisa viongozi hao.

Rais Xi Jinping na wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi walihudhuria mkutano huo.

Wajumbe wa bunge hilo pia wamewaidhinisha kwa kuwapigia kura wenyeviti, manaibu wenyeviti na wajumbe wa kamati maalum nane za Bunge la Umma la 14 katika mkutano huo.

Manaibu mawaziri wakuu, makansela na Katibu Mkuu wa Baraza la Serikali la China wamekula kiapo cha kutii Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China. 

Manaibu Mawaziri Wakuu, makansela wa nchi ya China na Katibu Mkuu wa Baraza la Serikali la China wakila kiapo cha kutii Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 12, 2023. Wakiwa wameteuliwa na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, na Ding Xuexiang, He Lifeng, Zhang Guoqing na Liu Guozhong wameidhinishwa kuwa manaibu mawaziri wakuu, wakati Li Shangfu, Wang Xiaohong, Wu Zhenglong, Shen Yiqin na Qin Gang wameidhinishwa kuwa makansela wa Nchi ya China, na Wu Zhenglong ameidhinishwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Serikali la China kwenye kikao cha tano cha wajumbe wote wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC). (Xinhua/Gao Jie)

Mawaziri wa Baraza la Serikali la China, wakuu wa kamati, Mkuu wa Benki Kuu ya China, na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali ya China wakila kiapo cha kutii Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China hapa Beijing, Machi 12, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

Wajumbe wa kamati maalum za Bunge la Umma la 14 la China (NPC) wakila kiapo cha kutii Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China hapa Beijing, Machi 12, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha