

Lugha Nyingine
China kuhimiza maendeleo ya ubora wa juu kwa nia thabiti
Mkutano wa Bunge la Umma la China, ambacho ni chombo cha juu zaidi cha kutunga sheria nchini China umefungwa leo hapa Beijing. Akiongea kwenye ufungaji huo, Rais Xi ambaye amechaguliwa tena kuwa rais wa China amesema imani ya wananchi kwake inamsukuma mbele, na pia imemletea majukumu makubwa, hivyo atafanya kazi kwa bidii, ili kuwaridhisha wananchi.
Rais Xi amesema, katika mchakato mpya wa ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawi wa taifa, China inapaswa kuendelea kuhimiza maendeleo ya sifa ya juu, kuzingatia zaidi wananchi siku zote, kushughulikia sambamba maendeleo na usalama, kuhimiza utekelezaji wa sera ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili” na Muungano wa Taifa , na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Kuhusu ujenzi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi amesema wakati wa kujenga nchi yenye nguvu kubwa, inapaswa kuimarisha kihalisi ujenzi wa Chama, na kupambana na ufisadi kwa nia thabiti , ili kutoa uhakikisho thabiti kwa ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawi wa taifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma