Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lafanya mkutano wa kamati ya kudumu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2023

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akihudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Kudumu ya Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC hapa Beijing, Machi 12, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

BEIJING - Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, Jumapili alasiri ilifanya mkutano wa kamati ya kudumu.

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC, na manaibu wenyeviti wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya CPPCC walihudhuria mkutano huo.

Washauri wakuu wa kisiasa walielezwa kuhusu rasimu ya uamuzi wa kuunda kamati maalum za Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC na kuhusu orodha ya rasimu ya wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wa kamati hizo maalum.

Rasimu hizo zilijadiliwa na kuidhinishwa kwenye kikao cha Baraza la Wenyeviti siku ya Jumapili asubuhi, ambacho pia kilipitisha kimsingi mpango kazi muhimu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC wa Mwaka 2023.

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akiongoza mkutano wa kwanza wa Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 12, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha