Waziri mkuu aeleza imani kubwa na ukuaji wa uchumi wa China

(CRI Online) Machi 13, 2023

Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang ameeleza imani kubwa na mustakbali wa uchumi wa China, akisema “utashinda upepo na mawimbi na kuwa wa kutarajiwa.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China kufungwa hii leo hapa Beijing, waziri mkuu Li alisema kuimarisha ukuaji wa uchumi ni kazi yenye changamoto si kwa China pekee bali kwa nchi zote duniani mwaka huu kutokana na sababu nyingi za kutokuwa na uhakika na utulivu. China imeweka lengo la ukuaji wa uchumi wa kuwa asilimia 5 kwa mwaka kutokana na sababu mbalimbali, na utimizaji wake hautapatikana kwa urahisi na unahitaji juhudi kubwa.

Ameeleza kuwa China itatumia vyema sera kambabe ikiwa ni pamoja na sera kuu, kupanua mahitaji, kuendeleza mageuzi na uvumbuzi, na kuzuia na kupunguza hatari zinazoweza kutokea, wakati huohuo nchi ya China itaongeza, kurekebisha na kuboresha sera katika mchakato wa utekelezaji.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha