Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China wafungwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2023

Xi Jinping na viongozi wengine wa China wakihudhuria kikao cha kufunga Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 13, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC), ambalo ni Bunge la Taifa la China umefungwa jana, Jumatatu asubuhi.

 Xi Jinping, Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi pamoja na Han Zheng walihudhuria kikao hicho cha kufunga mkutano, ambacho kiliongozwa na Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la 14 la China.

Akihutubia kikao hicho, Rais Xi Jinping amesema kuwa imani ya wananchi ndiyo motisha kubwa inayomhimiza kusonga mbele na jukumu kubwa analobeba.

Rais Xi amesema kuwa, atatekeleza kwa uaminifu majukumu yake yaliyotolewa na Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China, huku mahitaji ya Taifa la China yakiwa ndiyo dhamira yake na masilahi ya watu yakiwa ndiyo kipimo chake.

Ameahidi kutekeleza wajibu wake kwa umakini, kufanya kila awezalo, na kuthibitisha kuwa anastahili kuaminiwa na wajumbe wote wa Bunge la Umma la 14 la China na watu wa China wa makabila yote.

Rais Xi amesisitiza kuendeleza bila kuyumbayumba maendeleo yenye ubora wa juu, kuwaweka watu kwenye kipaumbele cha juu katika safari mpya, kuratibu vyema maendeleo na usalama wa China, kuendeleza utekelezaji wa "nchi moja, mifumo miwili" na lengo la Muungano wa Taifa, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Pia amesisitiza kushikilia uongozi wa CPC na uongozi wa juu wa pamoja wa serikali kuu.

Spika wa Bunge la Umma la China (NPC) Zhao Leji, akiunga mkono hotuba ya Rais Xi, ametoa wito wa kusoma kwa makini na kutekeleza maagizo ya Rais Xi, wakati akihutubia kikao hicho cha kufunga mkutano wa mwaka. 

Kikao cha kufunga Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 13, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

Xi Jinping akiwapungia mkono wajumbe wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 13, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

Xi Jinping akiwapungia mkono wajumbe wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 13, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

Xi Jinping na viongozi wengine wa China wakikutana na wajumbe wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) na kupiga picha pamoja nao baada ya kikao cha kufunga Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 13, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha