

Lugha Nyingine
Mabaki ya mpunga wenye umri wa miaka 1,300 yagunduliwa katika eneo la kale la Tibet
![]() |
Picha iliyopigwa kwa simu ya mkononi Tarehe 15 Mei 2021 ikionyesha mandhari ya eneo la Gyironggou katika Wilaya ya Gyirong, Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Shen Hongbing) |
LHASA, - Watafiti wa China wamegundua punje za mpunga wa indica kwenye eneo la kiakiolojia katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini-Magharibi mwa China, ikiashiria kwamba spishi hii ndogo ya mpunga ilienea hadi kwenye Uwanda wa Qinghai-Tibet karibu miaka 1,300 iliyopita.
Ugunduzi huo umefanywa na timu ya watafiti katika utafiti wake wa pili wa kina wa kisayansi uliofanyika kwenye Uwanda wa Qinghai-Tibet.
Watafiti hao walipokuwa wakisafisha sehemu katika eneo la Kongsangqiao katika Wilaya ya Jilung, iliyoko Mji wa Xigaze, walichimbua vipande kadhaa vya vyungu, baadhi ya vipande vya mifupa ya wanyama, na idadi kubwa ya mabaki ya mimea.
"Tumegundua nafaka za mpunga zilizochomwa kati ya mabaki ya mmea, ambazo kimofolojia zinakaribia kufanana na spishi ndogo za indica," amesema Gao Yu, mtaalam kutoka timu hiyo ya utafiti na mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Uwanda wa Tibet (ITP) ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China.
Wakati huo huo, mpangilio wa jeni wa mpunga wa indica pia ulipatikana katika DNA ya zamani iliyopatikana kutoka kwenye eneo la utafiti, ikithibitisha zaidi kuwa ni mpunga wa indica, mtafiti huyo ameongeza.
"Muda wa matokeo ya radiocarbon unaonyesha kwamba mabaki ya nafaka yanatoka katika Enzi ya Tang ya mapema (618-907),” amesema Gao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma