Umoja wa Mataifa wachukulia makubaliano kati ya Saudi Arabia na Iran yaliyofikiwa chini ya upatanishi wa China kuwa ni fursa kwa Yemen

(CRI Online) Machi 16, 2023

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Iran yaliyofikiwa chini ya upatanishi wa China ni fursa katika kutatua migogoro nchini Yemen.

Mapema siku hiyo, mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Bw. Hans Grundberg alikaribisha makubaliano hayo kwenye ujumbe wake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema mazungumzo hayo na uhusiano wa ujirani mwema ni muhimu sana kwa kanda nzima na Yemen, ambapo pande husika lazima zitumie fursa hiyo vizuri ili kuelekea kwenye mustakabali wenye amani zaidi.

Yemen imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Mwaka 2014 wakati Kundi la Wanamgambo wa Houthi linaloungwa mkono na Iran liliposhambulia miji kadhaa Kaskazini mwa Yemen, na kulazimisha serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia kuondoka mji mkuu wa Sanaa. Baadaye jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia liliingilia kati mgogoro huo na kuanza kupambana na waasi hao.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha