Putin atuhumu Marekani kuhusika na "shambulio la kigaidi" kwenye mabomba ya Nord Stream

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2023

Picha iliyotolewa na Walinzi wa Pwani wa Sweden Septemba 27, 2022 ikionyesha uvujaji wa gesi kutoka Bomba la Nord Stream kwenye Bahari ya Baltic. (Walinzi wa Pwani wa Sweden/Kitini kupitia Xinhua)

MOSCOW - Rais wa Russia Vladimir Putin Jumanne amesema, hoja kuhusu wapiganaji wanaoiunga mkono Ukraine walihusika katika mlipuko wa mabomba ya Nord Stream mwaka jana ni "upuuzi mtupu," akilaumu Marekani inahusika na kile alichokiita "mashambulizi ya kigaidi."

"Lazima tuwatafute wale ambao wana nia. Kinadharia, Marekani ina nia ya kusimamisha usambazaji wa nishati ya Russia kwenye soko la Ulaya ili kusambaza yake, ikiwa ni pamoja na LNG (gasi asilia ya kimiminika), hata kama ni asilimia 25-30 ya gharama kubwa zaidi kuliko Russia," Putin amesema kwenye mahojiano na kipindi cha televisheni ya Russia.

"Ni changamoto kwetu kufanya uchunguzi wetu wenyewe ikiwa hatutaruhusiwa kufika eneo la shambulio hili la kigaidi. Ukweli kwamba hili ni shambulio la kigaidi siyo siri tena kwa mtu yeyote. Kwa maoni yangu, kila mtu tayari amelitambua hili. Zaidi ya hayo, shambulio la kigaidi lilifanywa wazi katika ngazi ya serikali kwa sababu hakuna watu wa kawaida wanaweza kufanya vitendo kama hivyo, "Putin amesema.

"Mlipuko wa aina hii, wa nguvu kama hiyo, kwa kina kama hicho unaweza kufanywa tu na wataalamu na kuungwa mkono kwa nguvu zote za nchi yenye teknolojia fulani," ameelezea.

Russia iliomba Serikali ya Denmark kuangalia mabomba ya Nord Stream kwani vifaa vya vilipuzi bado vinaweza kupandikizwa huko, lakini "jibu lilikuwa lisilo wazi ... Walisema kwamba inabidi tusubiri," Putin amesema.

Katika makala iliyochapishwa mwezi uliopita, mshindi wa Tuzo ya Pulitzer Seymour Hersh alifichua kuwa Marekani ilishirikiana na Norway katika operesheni ya siri Juni 2022 ya kutega vilipuzi vilivyorushwa kwa kutokea mbali ambavyo vililipua mabomba matatu kati ya manne ya Nord Stream miezi mitatu baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha