Watanzania zaidi ya laki nne kunufaika na mradi wa maji wa Ziwa Victoria

(CRI Online) Machi 17, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya Mkoa wa Tabora Bw. Mayunga Kashilimu amesema watu wasiopungua 430,000 katika miji mitatu ya Mkoa wa Tabora, Magharibi mwa Tanzania watanufaika kutokana na mradi wa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria.

Akiongea na wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Kashilimu amesema mradi huo unaotekelezwa kwenye miji 28 nchini Tanzania utakamilika Mwaka 2025, na ni moja ya miradi mikubwa ya Tanzania.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha