Wizara ya Ulinzi ya China yaapa kutoacha nafasi kwa shughuli za makundi yanayotaka “Taiwan ijitenge” na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Tan Kefei Alhamisi amesema Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) litalinda kwa uthabiti mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya nchi hiyo, na halitaacha nafasi kwa shughuli za aina yoyote za makundi yanayotaka "Taiwan ijitenge" na China.

Tan ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu vitendo vya uchochezi vya hivi karibuni vya Marekani, ambavyo vimezidisha mvutano kwenye Mlango Bahari wa Taiwan.

“Chanzo kikuu cha kuongezeka kwa mvutano kwenye Mlango Bahari wa Taiwan ni vitendo vya uchochezi vya mamlaka ya Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo cha Taiwan kushirikiana na vikundi vya nje katika kutafuta "Taiwan ijitenge," na azimio lao la ukaidi la kusimama dhidi ya masilahi ya kimsingi ya Taifa la China,” Tan amesema.

Ni haki kwa PLA kufanya operesheni za kijeshi katika kukabiliana na kuingiliwa kati na nchi za nje na shughuli za kujitenga zinazotafuta " Taiwan ijitenge," Tan ameongeza.

Taiwan ni Taiwan ya China, na suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China na kiini cha maslahi ya msingi ya China, Tan amesema, huku akisisitiza kwamba suala la Taiwan ni mstari wa kwanza mwekundu ambao hauruhusiwi kuvukwa katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Tan amesema China inapinga vikali aina yoyote ya mabadilishano rasmi au mawasiliano ya kijeshi kati ya Marekani na Taiwan, na inapinga kwa uthabiti Marekani kupandisha hadhi uhusiano wake mkubwa na Taiwan kwa namna yoyote ile.

"Tunaitaka Marekani kuachana na jaribio lake la kutumia Taiwan kuidhibiti China, na kusitisha 'mbinu zake za soseji za salami' na kuchukua hatua zaidi kuhusu suala la Taiwan," Tan amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha