China yatoa mpango wa kuleta mageuzi katika vyombo vya chama na serikali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023

BEIJING - Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali la China zimetoa mpango wa mageuzi ya vyombo vya chama na serikali, na kutoa uarifu wa kutaka mpango huo utekelezwe kwa uaminifu.

Mpango huo unasema, tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, juhudi zimefanywa ili kuvifanyia mageuzi zaidi vyombo vya chama na serikali, na kusababisha mageuzi ya kimfumo na ya jumla ya majukumu yao.

“Hata hivyo, uanzishwaji wa kitaasisi na mgawanyo wa majukumu ya vyombo hivyo vya chama na serikali bado haujafanyiwa mageuzi kikamilifu kwa kazi mpya,” mpango huo umeeleza, na kuongeza kuwa mageuzi na marekebisho zaidi yanahitajika.

Mpango huo unaeleza kuwa lengo la kuvifanyia mageuzi vyombo vya chama na serikali ni kujenga mfumo wa kiutendaji wa vyombo vya Chama na Serikali unaokamilishwa, unaofuata taratibu na wenye ufanisi mkubwa.

Mpango huo unaorodhesha mageuzi kadhaa kwenye vyombo vya Kamati Kuu ya CPC kama vile kuundwa kwa Kamati Kuu ya Mambo ya Fedha ili kuimarisha uongozi wa pamoja wa Kamati Kuu ya CPC kuhusu kazi ya fedha. Aidha, vyombo vingine ndani ya Kamati Kuu ya CPC vitakavyoundwa ni pamoja na Kamati Kuu ya Sayansi na Teknolojia, Idara ya kazi za kijamii na Ofisi ya kazi kuhusu Hong Kong na Macao.

Kuhusu kuimarisha mageuzi ya vyombo vya Bunge la Umma la China (NPC), mpango huo unasema kwamba kamati ya kazi inayohusiana na wajumbe wa bunge hilo itaundwa.

Juu ya kuimarisha mageuzi ya vyombo vya Baraza la Serikali la China, mpango huo unasema Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China itafanyiwa mageuzi. Aidha, vyombo kama vile Idara ya Kitaifa ya Udhibiti wa Fedha, Idara ya Kitaifa ya Takwimu, na kazi za Wizara ya Kilimo na Vijiji zitaboreshwa.

Mpango pia pamoja na mambo mengine mengi unaeleza juhudi za kuboresha utaratibu wa kazi ya kutunza wazee na utaratibu wa usimamizi wa haki miliki ya ubunifu.

Mamlaka za Serikali Kuu zinatarajiwa kukamilisha mageuzi hayo mwishoni mwa Mwaka 2023 huku zile za serikali za mitaa zikitarajiwa kukamilisha mageuzi hayo ifikapo mwishoni mwa Mwaka 2024, kwa mujibu wa mpango huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha