Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akutana na Ofisa Mkuu wa Hong Kong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023

Qin Gang, mjumbe wa taifa ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi ya China akikutana na John Lee, Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong ya China (HKSAR), hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, ili kubadilishana maoni yao juu ya kazi ya kidiplomasia inayohusiana na Hong Kong, Machi 16, 2023. (Xinhua)

BEIJING – Qin Gang, mjumbe wa taifa ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi ya China, Alhamisi amekutana na John Lee, Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong ya China (HKSAR), hapa Beijing ili kubadilishana maoni yao juu ya kazi ya kidiplomasia inayohusiana na Hong Kong.

Lee ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje ya China kwa msaada wake kwa Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong ya China kwa miaka mingi, haswa katika suala la kupinga uingiliaji kati wa nchi za nje, kufuata sera ya "nchi moja, mifumo miwili," na kukuza mabadilishano na ushirikiano wa nje wa Hong Kong.

Ameeleza matumaini yake kwamba wizara hiyo itaendelea kutoa mwongozo na msaada kwa Hong Kong katika maswala ya mambo ya nje yanayohusiana na Hong Kong.

“Wizara daima imekuwa ikiunga mkono serikali ya mkoa wa Hong Kong katika kuisimamia Hong Kong kwa mujibu wa sheria, na katika kutekeleza kikamilifu na kwa uaminifu sera ya "nchi moja, mifumo miwili," Qin amesema.

"Tutafuata mwongozo wa Fikra ya Xi Jinping kuhusu Diplomasia, kuendelea kuunga mkono, kuongoza na kusaidia Hong Kong katika kazi ya kidiplomasia inayohusiana na Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong na kulinda kwa uthabiti mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya China, hivyo kukuza ustawi na utulivu wa muda mrefu wa Hong Kong," Qin amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha