Wanariadha wa mbio za Marathon wa China wavunja rekodi iliyodumu kwa miaka 15

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023

Mbio za Marathon za Wuxi Mwaka 2023 zimefanyika kwenye Mji wa Wuxi wa China tarehe 19 mwezi huu, ambapo mwanariadha wa Kenya Enock ONCHARI amenyakua ubingwa wa mbio hizo kwa wanaume na kuweka rekodi mpya ya mbio hizo kwa kukimbia kwa saa 2 dakika 7 na sekundi 19, huku wanariadha wa China He Jie na Yang Shaohui kwa pamoja wakivunja rekodi ya Mbio za Marathon kwa wanaume nchini China iliyodumu kwa karibu miaka 15 na miezi 5. He Jie ameshinda nafasi ya pili, akiweka rekodi mpya ya kukimbia kwa saa 2 dakika 7 na sekundi 30.

He Jie, Yang Shaohui pamoja na bingwa wa mbio kwa wanawake Bai Li wote wamefuzu kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris na Michezo ya Dunia ya Budapest. 

Mwanariadha wa China He Jie aliyeshinda nafasi ya pili akishangilia baada ya mashindano ya wanaume ya Mbio za Marathon za Wuxi 2023 huko Wuxi, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China Tarehe 19, Machi, 2023. (Xinhua/Yang Lei)

Mwanariadha wa Kenya Enock Onchari akishangilia wakati wa mashindano ya wanaume ya Mbio za Marathon za Wuxi 2023 huko Wuxi, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China Tarehe 19, Machi, 2023. (Xinhua/Yang Lei)

Mwanariadha wa China Bai Li akipita mstari wa mwisho wakati wa mashindano ya wanawake ya Mbio za Marathon za Wuxi 2023 huko Wuxi, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Tarehe 19, Machi, 2023. (Xinhua/Yang Lei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha